Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mwasiti amefunguka sababu ya kutoshirikiana na wasanii wa kike kwenye kazi zake za muziki.

Mwasiti amesema kuwa uamuzi wake wa kufanya kolabo nyingi na wasanii wa kiume kwanza unatokana na ukweli kuwa anaweza kuwavuta mashabiki wa kike na wa kiume kwenye wimbo wake wa mapenzi.

Pia Mwasiti amesema kuwa kuna ugumu kuwashirikisha wasanii wa kike wa Tanzania kwa sababu huwa na mambo mengi wakati wa kufanya kazi.

Mwasiti amesema kuwa sababu nyingine ni gharama za mahitaji ya wasanii wa kike limejificha ndani ya sababu hiyo kwani mwenye wimbo ndiye anayehusika na gharama zote.

Aliongeza kuwa sababu za wasanii wa kike kutoshirikishana kwa wingi zimekuwa zikitajwa mara kwa mara na wasanii hao kwenye vyombo vya habari na ndivyo zilivyo, huku akikataa kuzirudia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *