Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mwana FA amesema kuwa amesukumwa kugombea Ubunge  jimbo la Muheza kutokana na kero mbili ambazo ni tatizo la barabara na maji.

Mwana Fa ambeye jina lake halisi ni Hamisi Mwinjuma amesema kuwa kero hizo zimesaababisha ya yeye kuomba ridhaa ya kugombea ubunge jimbo hilo la Muheza mkonai Tanga.

FA amesema kuwa kero hizo ni za muda mrefu zimekuwa ni tatizo sugu kwa wananchi ambazo ni changamoto kubwa katika jimbo hilo.

Amesema kuwa barabara ya Muheza hadi Amani yenye urefu wa kilometa 35 ambayo ipo katika kiwango cha changarawe ambayo kwa kipindi cha mvua huwa haipitiki, itakuwa ni kipaumbele chake katika utekelezaji wa majukumu yake.

Pia kuhusu maslahi ya wasanii amesema atahakikisha atatetea mahitaji ya wasanii kwa ujumla akiwa bungeni, atakuwa mmoja kati ya watunga sheria,hivyo wasanii hatowaangusha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *