Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amesema kuwa wakati anahaso kutoka kimuziki alikatishwa tamaa mno hasa alipokuwa anajitoa kwenye Lebo ya Wasafi chini ya Diamond Platnumz.
Harmonize amesema kuwa “Usiruhusu mtu akwambie kwamba huwezi, amka na uzifuate ndoto zako. Nitazame mimi, nilipoanza safari yangu ya muziki.
Kila mmoja alikuwa akinikejeli kwamba nitafanya nini kwenye kiwanda cha muziki? Nikawaambia nitafanya nitakachoweza kufanya.
“Na nilipotoka kwenye lebo yangu ya zamani (WCB) kila mmoja alikuwa akisema nimeisha, nitakufa Kimuziki. Nitazame sasa hivi, mimi ni mshindi. Na Konde Gang ni lebo namba moja Tanzania kwa sasa, Afrika Mashariki na tunaitafuta Afrika sasa hivi.”