Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Hamis Kigwangalla amesema kuwa hakuweza kuyataja hadharani majina ya wanaojihusisha mapenzi ya jinsia moja (Mashoga) kutokana na ushauri aliopewa na jamii inayomzunguka.

Dkt. Kigwangalla amesema hayo wakati akiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Ustawi wa Jamii Duniani ambayo kitaifa imefanyika jijini Dar es Salaam.

Katika maadhimisho hayo Kigwangalla ameeleza kuwa kufanya mapenzi ya jinsia moja ni kosa kibaiolojia na hairuhusiwi mtu kuvutiwa na mtu wa jinsia yake.

Naibu waziri huyo amesema katika sheria iliyotungwa mwaka 2012 ya kukazia adhabu ya mapenzi ya jinsia moja, kuna kipengele kinachotaka mtu achukuliwe hatua endapo ikithibitika amekaa mapozi yasiyoeleweka na ikabainika kuwa ni kwa lengo la mapenzi ya jinsia moja atafunguliwa mashtaka.

Pia Dkt. Kigwangalla amewaonya wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja na kusisitiza kwamba serikali inawachukulia hatua kimya kimya.

Mwezi uliopita Naibu waziri huyo alisema kuwa atataja orodha ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja (Mashoha) ili sheria ichukue mkondo wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *