Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Aslay amesema kuwa kwa sasa ameamua kuwa bize na mambo yake kwa sababu haoni faida ya kuwa na mwanamke maishani mwake.

Kauli ya mwanamuziki imejili baada ya kutoonekana na mwanamke wa aina yoyote hivi karibuni hivyo kumeibuka minong’ono kwa baadhi ya mashabiki wake na wadau wa muziki nchini.

Aslay ambaye aliachana na mpenzi wake wa muda mrefu aliyezaa naye mtoto mmoja Tessy Chocolate anasema kwa sasa anafurahi maisha hayo kwa sababu hana mawazo ya mapenzi.

Pia amesema kuwa kwa sasa ninafurahi sana kuishi maisha ya peke yangu, ninafanya kile ambacho ninakipenda, hakuna anayenipangia maisha. Kwa sasa bado niponipo kwanza, sina haraka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *