Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Aslay amefunguka sababu iliyomfanya aondoke kwenye nyumba ya kituo cha Mkubwa na Wanawe ambapo alipokuwa anaishi Waimbaji wenzake.
Aslay amesema kuwa hakuna matatizo yoyote yaliyomsababisha kuondoka katika kituo hicho bali aliamua kuifuata familia yake ili aweze kuishi nayo kwa ukaribu, tofauti na watu wengi wanavyofikiria.
Mkali huyo kutoka Yamoto Band kwasasa anatamba na wimbo wake unaokwenda kwa jina la ‘Angekuona’ ambao unafanya vizuri kwenye vituo vya radio na Tv nchini.
Muimbaji huyo ameongeza kuwa zamani alijisahau zaidi katika muziki, lakini kwa sasa amepanga kujibrand yeye mwenyewe na kuachia nyimbo zake mwenyewe ambazo zitamtambulisha zaidi.
Aslay licha ya kuwa Yamoto Band lakini kwasasa anaonekana kujikita kufanya kazi peke yake bada ya kundi hilo kuwa kimya kwa zaidi ya miezi sita.