Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba ametaja sababu zilizompelekea kushiriki tamasha la mwimbaji, Faustina Charles Mfinanga maarufu kama Nandy, ‘Nandy Festival 2021’ Mkoani Kigoma.

Kiba kupitia ukurasa wake wa twitter alieleza kuwa, bidii ya Nandy wa wasanii wa kike wenye uthubutu kama wake ni moja ya sababu zilizompeleka kuwa kati ya watakaotoa burudani kwenye tamasha hilo litalofanyika Juni 05 2021.

Nandy pia ataongozana na Baba Levo, Marioo, Mabantu, Baddest 47, Whozu, Linex, Dulla Makabilla, Stamina na wasanii wengine kibao na tamasha hilo litafanyika katika uwanja wa Mwanga Centre.

“Sanaa yetu ina upungufu wa wasanii wa kike, inabidi waliopo wapewe nguvu ili waweze kufanikiwa zaidi”.

“Nandy ni msanii anayejituma na mwenye jitihada. Napenda anachofanya na ndio maana Jumamosi ijayo nitaenda nyumbani Kigoma kumpa support katika Nandy Festival” ameandika Alikiba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *