Ofisi ya mashitaka nchini Rwanda imetangaza kuanza upelelezi kuhusu askari 20 wa nchi ya Ufaransa katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.

Tangazo lililotolewa na ofisi ya mashitaka ya Rwanda linasema kwamba Rwanda imewasilisha maombi ya ushirikiano wa kisheria ili askari watuhumiwa waweze kuhojiwa na wapelelezi wa Rwanda.

Katika tangazo hilo Rwanda inasema kuwa imeanza rasmi mchakato wa kisheria kuhusu maafisa hao wanaotuhumiwa hukusika moja kwa moja katika mauaji ya kimbari.

Mwendesha mashitaka mkuu wa Rwanda Richard Muhumuza alimwandikia mwezake wa Ufaransa Jean Claude Marin kutaka ushirikiano wa kisheria kuwasaidia wapelelezi wa Rwanda kuwahoji maafisa hao wa Ufaransa kupitia ubalozi wa Rwanda mjini Paris.

Maafisa hao 20 ni miongoni mwa askari wa Ufaransa waliokuwa katika kazi mbali mbali nchini Rwanda kuanzia mwaka 1990 hadi mwaka 1994.

Rwanda inawatuhumu kulisaidia jeshi la rais wa zamani Juvenal Habyarimana kwa silaha na kutoa mafunzo kwa wanamgambo wa Interahamwe waliotekeleza mauaji ya kimbari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *