Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ruby amesema kuwa amechoshwa na kile alichodai ni kuulizwa habari za Nandy kila siku anapohojiwa na watangazaji.
Ruby na Nandy wanasemekana kuwa wana bifu la chinichini ingawa wawili hao wamekanusha habari hizo.
Ruby alifunguka hayo kwenye kwenye mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni na stesheni moja ya redio na kudai kuwa amechoshwa na watangazaji wa media mbali mbali badala ya kumuuliza maswali ya maana kila siku wamekalia kumuuliza habari za Nandy ambazo kwa sasa zimeshamchosha na ni kitu kinachotengeneza ugomvi baina yao hata kama hakuna ugomvi.
Nachukia sana swali la kufananishwa na Nandy Kwa sababu honestly I am tired of that question! ni kama vile watangazaji wanashindwa ni maswali gani ya kuuliza , maswali ni yale yale nimeshayajibu sana ! I love Nandy she is a good artist, she is a good singer but don’t ask me too much questions about her, it’s like mnataka kutengeneza ugomvi sasa nashindwa kuelewa hata watu wa media mnatengeneza ugomvi sasa kwasababu swali lilishajibiwa mara Mia moja sasa kwa nini lijirudie kila siku?”.
Nandy na yeye alipoulizwa mara ya mwisho kama ana ugomvi na Ruby amesema hana tofauti na msanii huyo.