Mwanamuziki wa Rap Bongo, Rosary Robert ‘Rosa Ree’ amekiri kulia kwa ajili ya mapenzi hapo zamani.

Ree anasema kuwa, sababu ya yeye kulia ni kitendo cha kuwa na mpenzi aliyekuwa akimsaliti wakati yeye alikuwa akimuamini kinoma hivyo hakuweza kuamini alichofanyiwa.

“Mapenzi yanauma asikwambie mtu, mimi nilishawahi kulia kwa ajili ya mpenzi wangu ambaye alini-chit (kusaliti). Nilikuwa nikimuamini sana,” anasema Ree.

Mwanamuziki huyo kwasasa ni miongoni mwa wasanii wa kike wanaofanya vizuri nchini kutokana na ubora wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *