Mshambuliaji wa Everton, Wayne Rooney ametangaza kustaafu soka la kimataifa baada ya kukataa kushirikishwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kitakachomenyana katika mechi za kufuzu kombe la dunia.
Mshambuliaji huyo wa Everton aliombwa na kocha wa timu ya Uingereza, Gareth Southgate kushiriki katika mechi dhidi ya Malta na Slovakia.
Ronney amesema kuwa ”Kila mara nilipochaguliwa ilikuwa fahari kubwa kwangu lakini naamini imefikia muda wa kujiondoa”.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United alifunga mabao 53 katika mechi 119 za timu ya taifa.
Rooney ambaye hakushirikishwa na Southgate katika mechi dhidi ya Scotland na Ufaransa mnamo mwezi Juni alianza kuichezea Uingereza mwaka 2003 katika mechi ambapo Uingereza ilipoteza kwa Australia.