Mshambuliaji wa nyota wa Real Madrid na Ureno, Cristiano Ronaldo ameuza tuzo yake ya mchezaji bora wa dunia mwaka 2013 (Ballon d’or).
Ronaldo amesema dhamira yake ya kuuza tuzo hiyo ni kukamilisha hitaji la moyo wake ambalo ni kujitolea kusaidia watoto wenye magonjwa hatari.
Tayari tuzo hiyo imenunuliwa na tajiri aitwaye Idan Ofer kutoka Israel kwa kiasi cha €600,000 sawa na bilioni 1.583 za Kitanzania.
Ronaldo tayari ametwaa tuzo 4 za Ballon d’or ya kwanza ikiwa ni mwaka 2008 akiwa Manchester United na 2013 tuzo yake ya kwanza akiwa Real Madrid na ndio hiyo ameamua kuiuza ili kuchangia matibbau ya watoto.