Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia ya FIFA iliyotolewa jana mjini Zurich nchini Uswisi.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 31 amewashinda Lionel Messi wa Barcelona na Antoine Griezmann wa Atletico Madrid katika sherehe zilizofanyika mjini Zurich, Uswisi usiku wa jana.

cr74

Mchezaji huyo pia alishinda tuzo ya Ballon d’Or mwezi Disemba mwaka jana, kufuatia mafanikio yake katika Klabu Bingwa Ulaya akiwa na Real Madrid, na pia kushinda Euro 2016 akiwa na timu ya taifa ya Ureno.

Kwa upande mwingine kocha wa Leicester City, Claudio Ranieri ameshinda tuoz ya kocha bora wa mwaka kwa upande wa wanaume, huku Silvia Neid, meneja wa zamani wa Ujerumani akishinda kwa upande wa wanawake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *