Maandamano makubwa yanaendelea nchini Romania kupinga Serikali kupitisha sheria ya kuhalalisha baadhi ya matendo ya rushwa.

Maelfu ya watu wamekusanyika katika viunga vya mji wa Bucharest na miji mingine nchini humo kupinga sheria hiyo walioiita kandamizi.

Zaidi ya watu robo milioni waliandamana siku ya Jumatano yakiwa ni maandamano makubwa tokea kuanguka kwa utawala wa kikomunisti mwaka 1989.

Waziri mkuu wa nchi hiyo Sorin Grindeanu amesema kuwa Serikali haitabadilisha maamuzi hayo yaliyopitishwa.

Waandamanaji nchini Romani
Waandamanaji nchini Romani

Kwa upande mwingine Rais nchi hiyo Klaus Iohannis amesema ataishauri mahakama kuhusiana na suala hilo.

Kupitia sheria hiyo, viongozi mafisadi hawatapelekwa mahakamani kama kesi zao zitahusisha ufujaji wa fedha chini ya dola elfu 48 za Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *