Muongozaji wa filamu Roman Polanski amejiondoa kwenye jopo la majaji wa tuzo za Cesars za nchini Ufaransa kufuatia mashabiki kuonyesha waziwazi kukerwa na kuchaguliwa kwake.

Tangu kuchaguliwa kwake wiki iliyopita, mashabiki na vyama vya wanawake vimeonyesha hasira zao ikiwa ni pamoja na kuitisha maandamano kupinga kuonyeshwa kwa utolewaji wa tuzo hizo unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.

Mwanasheria wake, Herve Temime ametoa taarifa ya kujiondoa kwenye wadhifa huo kwa muigizaji huyo wa zamani na kusema ‘utata, umemsikitisha sana Roman Polanski na umeiathiri familia yake’.

‘Hata hivyo, ili kutoharibu sherehe za utoaji tuzo za Cesars, ambazo zinapaswa kuangalia sinema na sio uteuzi wa rais (French Academy of Cinema Arts and Techniques), Roman Polanski ameamua kukataa mualiko na hatoongoza utoaji ujao wa tuzo za Cesars’.

Sherehe za utoaji wa tuzo hizo za 42 za Cesars zitafanyika jijini Paris mnamo February 24

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *