Mwanamuziki wa Hip Hop, Roma Mkatoliki amevunja ukimya kuhusu maendeleo ya sanaa ya muziki wa Bongo fleva nchini Marekani kwa madai ya kuwa muziki huo hajulikani kabisa.
Roma ameonyesha kushangazwa na kudorora kwa makuzi ya muziki huo nchini humo ukilinganisha na muziki wa mataifa mengine ya afrika ambayo walau yanapata nafasi.
“Shida ya huku tulipo, huwezi kwenda sehemu ya Starehe (Club) ukakuta ngoma za Bongo flava hata 2 tu zinapigwa, kuna muda unatamani uende Disco ukacheze hata Singeli lakini wapi!
Kinyonge mnarudi magetoni mna-connect Bluetooth Speaker mnasikiliza Wana! SEMA IPO SIKU TU WATAIJUA BONGOFLEVA.” Ameandika.
Roma ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter huku akihitimisha kwa kudhihirisha kuwa bado anamatumaini ya kuwa upo wakati muziki huo utafikia katika hatua ya kufahamika nchini humo.