Mwanamuziki wa Hip Hop nchini Roma Mkatoliki ameweka rekodi ya kushika namba 1 kati ya wasanii 10 wa Hip Hop Afrika Mashariki wenye wafuasi wengi katika mtandao wa YouTube.
Akitoa taarifa hiyo kupitia mitandao yake ya Instagram na Twitter, Roma Mkatoliki anaongoza kwa kuwa na wafuasi 265k.
Orodha ya wasanii wengine ambapo namba 2 imekwenda kwa Nyashinski 252k, Kenya 3. Darassa 240k, Tanzania 4. Khaligraph Jones 220k, Kenya 5. King Kaka 219k, Kenya 6. Nay Wa Mitego 180, Tanzania 7. Dogo Janja 161, Tanzania 8. Octopizzo 143k Kenya 9. Proffesor Jay 119k Tanzania 10. Young Killer 91k Tanzania.
Baada ya kushika orodha hiyo Roma amesema kuwa Hip Hop unaopendwa sana na watu na una mashabiki wengi sana, sina uhakika na hili,kwamba kwenye “Digital Platforms” hatuna wafuasi wengi ukilinganisha na aina nyingine za muziki, kwahiyo mimi kuwapata wafuasi 265K na kuwa namba 1 Afrika Mashariki na Kati, haikuwa rahisi hata kidogo, hii ni baraka”.
Mwanamuziki huyo kwasasa yupo nchini Marekani kikazi ambapo aliachia nyimbo mbili akiwa nchini humo hivi karibuni.