Nahodha wa Uholanzi, Arjen Robben ametanagza kustaafu soka la kimataifa baada ya Uholanzi kushindwa kufuzu kwa Kombe la Dunia nchini Urusi mwakani.
Robben alifunga mabao yote mawili katika ushindi wao wa 2-0 dhidi ya Sweden, lakini mabao hayo hayakutosha kuwafikisha michuano ya kufuzu kwa muondoano.
Robben amechezea taifa lake mara ya kwanza Aprili 2003 na kwa jumla amewachezea mechi 96 na kufunga mabao 37.
Anashikilia nafasi ya nne kwenye ufungaji wa mabao timu ya taifa ya Uholanzi, nafasi anayoishikilia kwa pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Dennis Bergkamp.
Uholanzi walihitaji kushinda kwa mabao saba wazi dhidi ya Sweden ili kuwapita Sweden na kumaliza nafasi ya pili kundi lao.
Robben alikuwa kwenye kikosi kilichomaliza cha tatu Kombe la Dunia 2014 na kikosi kilichoshindwa fainali 2010 na Uhispania.