Muigizaji wa Bongo Movie, Riyama Ally ameonyesha hisia zake juu ya tuzo za Sinema Zetu International Film Festival zilizofanyika wiki iliyopita baada ya Kukosa tuzo.
Tangu tuzo hizo zifanyike wiki iliyopita zimezidi kuwa gumzo kwani baadhi ya wasanii wa Bongo movie wameonyesha kutokuridhika baada ya kukosa tuzo na wasanii wengine kupata tuzo.
Wasanii kama Batuli na Irene Uwoya wameweka wazi kuwa hawajapendezwa na kitendo cha Wema kushinda tuzo ya msanii bora wa kike na kuamini kuna swankiest wengine wanaofanya vizuri kuliko wao kwenye tasnia hiyo.
Riyama Ally pia ni moja kati ya wasanii wa kike ambaye ameweka wazi kuwa anaamini alistahili kushinda tuzo hiyo.