Ndugu wa marehemu wa mwanafunzi aliyepigwa risasi na Polisi, Akwilina Akwilini wamepinga ripoti ya postmortem baada ya kuelezwa kuwa majibu ya ripoti ya kifo cha mwanafunzi huyo yatatolewa baada ya siku 14.

Ndugu hao waliokuwa wamekusanyika Muhimbili karibu na eneo la chumba cha kuhifadhia maiti wakisubili ripoti, wameeleza kusikitishwa kwao na uamuzi huo huku wakilalamika na kuhoji kwa nini wasipewe ripoti hiyo leo ili wakazike mwili wa ndugu yao.

Hali hiyo ilizua sintofahamu huku wengine wakikubali kuchukua mwili na wengine wakikataa wakitaka kupewa ripoti kamili ya uchunguzi wa kifo hicho.

Kwa upande wa Mkuu wa  Chuo cha NIT, Zakaria Mganilwa amesema uongozi wa chuo hicho umeungana na familia kuhakikisha wanampumzisha Akwilina.

Pia mkuu wa chuo huyo amesema kuwa anafanya jitihada za kuzungumza na madaktari na ndugu wa marehemu kufanikisha zoezi la kuchukua mwili na kwenda kuuzika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *