Mcheza Judo wa Misri Islam El Shehaby amerudishwa nyumbani kutoka kwenye mashindano ya Olimpiki yanayoendela nchini Brazil baada ya kukataa kumpa mkono mpinzani wake kutoka nchini Israel, Or Sasson baada ya pambano lao.
Mcheza Judo huyo alipewa onyo kali na kamati ya kimataifa ya Olimpiki, (IOC) baada ya kupigwa kwenye raundi ya kwanza kisha kukataa kumpa mkono mpinzani wake siku ya Ijumaa.
IOC imesema kuwa vitendo vya Islam vimeenda ‘kinyume na hali ya urafiki iliyopo kwenye michezo hii’
Kamati ya Olimpiki ya Misri imelaani kitendo cha mwanamichezo huyo na kimemrudisha nyumbani.
Hata hivyo mpinzani wake Sasson amesema kuwa alionywa na makocha wake kuwa huenda Islam akakataa kumpa mkono.