Mbunge wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani, Ridhwani Kikwete amesema kuwa ameitwa na kuhojiwa na kamisheni ya kupambana na dawa za kulevya na kukutwa hana hatia kuhusu tuhuma za kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya.
Kupitia akaunti yake ya Instagram Ridhwani Kikwete amesema ana shukuru haki imetendeka katika sakata hilo lililokuwa likimkabili.
“Ni kweli niliitwa na kuhojiwa. Serikali yangu chini ya Kamisheni ya Madawa ya kulevya inasimamia haki na nimeona ikitendeka. Niko huru toka kwenye tuhuma/kashfa,”
“Tuunge mkono juhudi hizi. Tuunge mkono hatua zinazochukuliwa ili kuokoa vijana wetu na kulinda nguvu kazi ya Taifa #vitadhidiyaMadawa #magufulinikazitu #tanzaniakwanza #miminikazitu #chalinzenikazitu,”.
Ridhwani ni miongoni mwa watu waliotajwa kwenye orodha ya majina 97 ya watuhumiwa wa biashara haramu ya dawa za kulevya ambayo RC Makonda alimkabidhi Kamishna wa kupambana na dawa za kulevya nchini, Rogers Sianga.