Mwanamuziki wa hip hop nchini Marekani, Rick Ross amewasili jijini Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya show nchini humo.

Rick Ross ametua mapema leo katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi ambapo amepokelewa na mashabiki pamoja na wadau wa muziki nchini Kenya ambao wameonesha kufuraishwa na ujio wa mwanamuziki huyo.

Baada ya kuwasili, Rick Ross amesema kuwa anafurahi sana kufika nchini Kenya kwani ndiyo mara yake ya kwanza kutua nchini humo.

Katika ukanda wa Afrika Mshariki hii ni mara ya pili kwa mwanzamuziki huyo kutua baada ya mara ya kwanza kutua nchini Tanzania kwenye Tamasha la Fiesta lililofanyika mwaka 2012.

Show hiyo ya Rick Ross nchini Kenya inatarajiwa kufanyika kesho katika ukumbi wa Carnivore Grounds na kusindikizwa na wasanii wa Kenya kama vile Khaligraph Jones na Nyansiski.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *