Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rich Mavoko amesema siyo kweli kwamba ana uhusiano wa kimapenzi la mwenzake, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’.
Mavoko amesema kuwa, ukaribu wake na Lulu Diva ndiyo ulisababisha watu kuanza kuzungumza hayo, lakini hakuna jambo kama hilo.
Mwanamuziki huyo amesema kuwa maisha yake yamekuwa binafsi sana tangu aanze muziki ndiyo maana watu wanajua ni Lulu Diva kwa sababu alikuwa naye karibu, lakini siyo mpenzi wake.
Kauli mwanamuziki huyo imekuja baada ya watu kuhoji ukaribu wa wa wawili hao kupelekea watu kuwahisi wana uhusiano wa kimapenzi jambo ambalo siyo la ukweli.
Rich Mavoko kwasasa amerudi tena kwenye muziki baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila ya kuachia ngoma yoyote lakini sasa amerejea kwa kuachia nyimbo zake mpya.