Klabu ya Real Madrid imevunja rekodi ya Barcelona baada ya kushinda mechi 16 kwenye ligi nchini Uhispania baada ya kuilaza Espanyol 2-0 kwenye mechi ya La Liga hapo jana.
Ushindi huo dhidi ya Espanyol unaifanya Real Madrid kuongoza ligi hiyo kwa tofauti ya alama tatu ambapo amefikisha alama 12 katika michezo minne iliyocheza hadi sasa ambapo wameshinda yote.
Mabao kutoka kwa James Rodriguez na Karim Benzema yaliwawezesha kufikia rekodi hiyo iliyowekwa na Barcelona walipokuwa chini ya Pep Guardiola msimu wa 2010-11.
Real Madrid walicheza bila nyota wao Gareth Bale na Cristiano Ronaldo ugenini uwanja wa Cornella-El Prat lakini hilo halikuwazuia kuandikisha ushindi wao wa nne kutoka kwa mechi nne walizocheza msimu huu.
Barcelona wanashikilia nafasi ya pili ligini kwasasa wakiwa na alama tisa, sawa na Las Palmas.