Shirikisho la soka duniani FIFA limetupilia mbali rufaa zilizowasilishwa na klabu za Real Madrid na Atletico Madrid za Hispania baada ya kufungiwa kufanya usajili hapo Januari mwaka huu.

 FIFA wamekataa rufaa za timu hizo iliyokuwa inafungia kufanya usajili katika madirisha yote mawili ya usali barani Ulaya kutokana na kukiuma kanuni za usajili.

Timu hizo zilifungiwa na kamati ya nidhamu ya FIFA mwezi Januari mwaka huu kutofanya usajili kwa madirisha mawili kutokana na kukiuka kanuni za usajili wa Shirikisho hilo baada ya kufanya usajili wa wachezaji wa chini ya miaka 18 wasio raia wa Hispania.

Adhabu hiyo wataanza kuitumikia kuanzia sasa kwani awali ilishindika kutokana na klabu hizo kukata rufaa.

Kutokana na adhabu hiyo hivyo klabu hizo hazitoruhusiwa kufanya usajili hadi January 2018 ambapo pia wamepigwa faini kutokana na kosa hilo

Real Madrid watatakiwa kulipa paundi 249,00 naAtletico Madrid  paundi 622,000, vilabu hivyo vinaweza kufanya usajili lakini havitaruhusiwa kuwatumia wachezaji hadi 2018.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *