Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla ametoa siku 14 kwa Halmashauri zote za mkoa huo kuwaondoa watu wote waliovamia hifadhi ya misitu pamoja hifadhi ya msitu wa mto Mbeya.
Makalla ametoa agizo hilo katika kilele cha upandaji miti kimkoa katika chanzo cha maji cha mto Hanzya kata ya Itagano jijini Mbeya.
Pia mkuu wa mkoa huyo ameitaka jamii kuwa na utamaduni wa kupanda miti ya vivuli na matunda ili kutunza vyanzo vya maji kwani kufanya hivyo kutasadia kutunza mazingira yetu yaliytuzunguka.
Kwa upande wake Afisa Misutu mkoa wa Mbeya, Joseph Butuyuyu amesema kuwa mpango wa kuhifadhi mazingira katika mto Mbeya umeanza kwa mafanikio makubwa toka walipoanzisha.