Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa majina ya awamu ya tatu wanaojihusisha na biashara haramu za dawa za kulevya imekamilika.

RC Makonda amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kusema kuwa anataka kuonana na waandishi wa habari leo Jumatatu hii katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere kuanzia saa 4 asubuhi.

Kupitia ukurasa wake Instagram ameandika  “Awamu ya tatu imekamilika naomba tukutane kesho katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere kuanzia saa 4 asubuhi.”

Mkuu wa mkoa anaendeleza vita aliyoanzisha ya madawa ya kulevya ambapo tayari ameshataja awamu mbili za majina wanaohusika na baishara hiyo haramu ya madwa ya kulevya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *