Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa wanawake 178 waliofika kwake kulalamikia kutelekezwa na baba za watoto wao, wamepatanishwa na wazazi wenzao.

Makonda amebainisha hayo alipokuwa anazungumzia mafanikio yaliyopatikana tangu kuanza kwa kampeni hiyo, Jumatatu iliyopita.

Makonda alisema, hatua hiyo ni nzuri kwa kuwa lengo kubwa la mkakati wake ni kusaidia upatikanaji wa haki ya kwanza ya watoto, ambayo ni malezi ikifuatiwa na haki nyingine kama vile upendo na ukaribu.

Pia Makonda aliweka wazi kuwa hadi sasa, wapo wanaume ambao wamekubali kupimwa vinasaba (DNA) ili kubaini uhalali wa watoto wanaoambiwa kuwa ni wao.

Siku ya jumatatu wanawake katika jiji la Dar es Salaam walijitokeza katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya malalamiko kuhusu kutelekezewa watoto na wanaume wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *