Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Khaled Mohamed (TID) amekutana na kufanya mazungumzo na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuhusu suala la madawa ya kulevya.

Katika mazungumzo ya wawili hayo walikuwa wanajadili kuhusu kuokoa vijana kutoka kwenye janga la madawa ya kulevya ambayo yamekuwa yakiondoa nguvu kazi ya taifa.

TID amesema kuwa muziki bila ya dawa za kulevya inawezekana kutokana na janga hilo kuhathiri wanamuziki wengi wa Bongo Fleva pamoja na tasnia zingine za sanaa hapa nchini.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa siku zote mungu ajalala yupo pamoja na vijana kwa hiyo atasaidia kwenye janga hilo la madawa ya kulevya.

TID ni miongoni mwa wasanii waliotajwa na Paul Makonda wanahojihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya ambao walifika kituo cha polisi na kukiri kama wanatumia madawa hayo na kuomba msaada.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *