Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda ameagiza kuvunjwa kwa baadhi ya nyumba maeneo ya Buguruni kwa Mnyamani zilizojengwa karibu ya mto Msimbazi ambazo zilikumbwa na mafuriko.

Makonda ametembelea maeneo hayo na kutoa agizo hilo baada ya kuona uharibifu mkubwa uliosababishwa na mvua iliyonyesha juzi jijini Dar es Salaam na kuwaamuru kuhama makazi hayo.

Pia Mkuu wa mkoa huyo alisikiliza kero za wananchi wa maeneo hayo na kuwahoji baadhi ya maswali huku akigusia sababu zinazosababisha wakazi hao kushindwa kuhama maeneo ya mabondeni.

Kwa upande mwingine Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewataka wananchi wanoishi maeneo ya mabondeni kuhama wenyewe kwa hiari kabla jeshi hilo alijachukua hatua za kisheria.

Kamishna wa Kanda hiyo, Kamanda Simon Sirro amesema kuwa wananchi waishio wanatakiwa kuhama maeneo hayo kutokana na kuatarisha maisha yao.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *