Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rayvanny ni miongoni mwa wasanii waliochaguliwa kuwania tuzo za Big Apple Music Awards kwenye kipengele cha ‘Best Tanzanian Musician.

Rayvanny anakuwa msanii Pekee kutoka Afrika Mashariki kutajwa katika tuzo hizo ambazo zinawakutanisha Wasanii mbalimbali wakubwa Duniani.

Wasanii wengine wanaowania tuzo hizo ni kama vile Selena Gomez, Nick Minaj na Dj Khaled Pamoja na Anitta na wengine wengi.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Staa huyo Ameandika Ujumbe na kusema kuwa alimuahidi Mh Rais Samia Suluhu Hassan kuwa hatoacha kuiwakilisha Nchi ya Tanzania Duniani kupitia Muziki wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *