Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rayvanny amewasili mkoani Mbeya kunogesha tamasha la ngoma za asili maarufu kama Tulia Traditional Dance lilionza jana.
Rayvanny amepokelewa na mwenyeji wake Mbunge wa Wanawake Mkoa wa Mbeya amabaye pia ni Naibu waziri wa Maji nchini Tanzania, Maryprisca Mahundi leo jioni.
Akiwasili katika viwanja hivyo amepokelewa na shamrashamra za ngoma za asili zikiwemo za kabila la Wasafwa ambalo ni maarufu kwa mkoa wa Mbeya.
Akizungumza baada ya kuwasili, Rayvanny amesema Mbeya ni nyumbani hivyo hatoweza kuwaangusha viongozi wa mkoa akiwepo Mbunge wa Mbeya Mjini ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson.
“Mimi Mbeya ni kwetu nilikuwa na shoo nyingine Dar Es Salaam lakini nimeona hapana nije nyumbani kufanya mambo na vijana wangu wa mbeya wananijua mambo yangu lengo pia ni kitangaza utalii wa ngoma zetu za asili” amesema.
Kwa upande wake Naibu waziri wa Maji nchini Tanzania, Maryprisca Mahundi amesema kuwa Tamasha hilo la ngoma za asili limeandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Dk Tulia Ackson na litahusisha ngomba za asili kutoka maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja ma viongozi mbalimbali na wadau.
Mhandisi Mahundi amewataka wananchi mkoani Mbeya kijitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo litakalohusisha vikundi mbalimbali.
Tamasha hilo ambalo linatarajia kushirikisha makabila zaizi ya 120 kutoka mikoa mbalimbali Tanzania litahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwepo Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa lengo likiwa ni kutangaza utalii wa ngoma za asili.