Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rayvanny ametajawa kuwa msanii pekee atayetumbuiza kwenye tuzo kubwa za muziki duniani zijulikanazo kama Mtvema ambazo kwa mwaka huu 2021 zitatolewa nchini Hungury.


Kwa mara ya kwanza Rayvanny atatumbuiza kwenye jukwaa hilo la tuzo za kimataifa akiwa na msanii kutoka nchini Columbia aitwaye Maluma ambaye amemshirikisha Rayvanny kwenye wimbo wao Mama Tetema ambao kwa mara ya kwanza utasikika kwenye tuzo hizo za MtvEma2021.


Taarifa hizo zimetolewa na ukurasa rasmi wa mtandao wa kijamii wa Twitter kupitia akaunti yao ya Mtv ema.

Maluma ni moja kati ya wasanii wanaofanya vizuri kwenye muziki wa Latin America akiwa na zaidi ya subscribers Milioni 27 kwenye mtandao wa YouTube, Followers zaidi ya Milioni 50 kwenye mtandao wa Instagram.


Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika mnamo November 14,2021 huko nchini Hungury huku Afrika Mashariki tukiwa tunawakilishwa na Diamond Platnumz ambaye ametajwa kwenye kipengele cha Best African Act.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *