Mwanamuziki wa Bongo Fleva kutoka lebo ya wasafi, Raymond Mwakyusa, Rayvanny amesema ikitokea nafasi ya kuchora tattoo atachora ya  mpenzi wake Paula  Kajala.

Rayvanny atoa kauli hiyo wakati akifanya mahojiano na kipindi cha Big Sunday Live jana baada ya kuonekana amechora tattoo ya lebo yake mpya.

Sababu ya kumtaja Paula ni baada ya kuulizwa maswali hukuhu mzazi mwenzake Fayvanny na mpenzi wake wa sasa  kuwa nani  anampa nafasi kubwa.

Hata hivyo amesema hawezi kuchagua kuwa nani anamkubali zaidi  kutokana na heshima anayowapa wote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *