Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rayvanny ameshangazwa na Muitikio wa Ngoma yake ya Chuchumaa namna inavyoendelea kufanya vizuri.
Rayvanny ameshangazwa kutokana na Ngoma yake hiyo kuwa na Takribani miaka 3 tangu iachiwe lakini hadi sasa inaendeea kufanya vizuri katika platform mbali mbali za muziki.
Ngoma hii mpaka sasa kwenye Mtandao wa Youtube ina watazamaji zaidi ya Milioni 12 toka ilipotoka miaka mitatu iliyopita.
Rayvanny kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema kuwa “MZIKI KITU CHA AJABU SANA YANI NIMEAMKA NAKUTA WIMBO WANGU WA CHUCHUMAA UNA TREND SEHEMU TOFAUTI TOFAUTI DUNIANI IMAGINE WIMBO UNA MIAKA 3.