Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rayvanny amewashangaa wanaomsema vibaya kuwa anajichubua kitendo ambacho hajawahi kukifikiria katika maisha yake.

Kauli ya mwanamuziki huyo imekuja baada ya baadhi ya watu kusema kuwa mwanamuziki huyo anajichubua kutokana na kuwa mweupe.

Rayvanny alisema kuwa anashangaa maneno hayo yanatoka wapi kwani katika maisha yake haja­wahi kuwaza kufanya hivyo na anachoamini yeye watu watakuwa wanaongea kwa sababu ya muonekano wake kwenye picha.

Ravanny amesema kuwa walimwengu hawakosagi cha kusema, unajua kuna picha ambazo zikitupiwa mtandao­ni naonekana mweupe sana na nyingine zinakuwa zime­toka vibaya, hapo watu ndiyo huanza kusema nimejichibua, kitu ambacho siyo kweli,” alisema Rayvanny.

Hivi karibuni msanii huyo aliposti picha kwenye akaunti yake ya Instagram akiwa ana­toka kwenye mahojiano na moja ya vyombo vya habari hapa nchini, ambapo picha hiyo ilionesha magoti yake ni meusi tofauti na sehemu nyingine za mwili wake hivyo kuwafanya wadau kudhani amejichubua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *