Mwanamuziki wa Bongo Fleva kutoka WCB, Rayvanny inasemekana ameachana na mpenzi wake Fahma ambaye pia ni mama wa mtoto wake Jayden.

Rayvanny na Fahima wamekuwa wakitawala vichwa vya habari katika siku za hivi karibuni na tetesi za wawili hao kuachana lakini mara kwa mara imekuwa mara tu baada ya habari hizo kuenea wawili hao wanaonekana tena pamoja.

Sakata hilo lilianza baada ya Rayvanny kupitia ukurasa wake wa Instagram kuweka ujumbe wenye utata ulioandikwa.

Mpende ila usimuamini, Mpe ila sio vyote mtunze ila usimchunge, mpe mwili wako ila usimpe siri zako Ata mkojo ulikuwa soda mwanzoni, utamu ndio vichungu, Keep it in your mind”.

Baada ya Rayvanny kuweka ujumbe huo uliibua maswali mengi kwenye vichwa vya watu kuhusu nini hasa alimaanisha kwa maneno yale au endapo alikuwa anampiga kijembe mpenzi wake. Lakini Fahima naye alijibu mapigo kwa kuweka picha hii;

Ambapo chini ya picha hiyo ilisindikizwa namaneno ‘Single mama’ yenye kumaanisha hana mpenzi anamlea mtoto wake mwenyewe.

Lakini mpaka sasa sio Rayvanny wala Fahima aliyeweka wazi kuwa wameachana au badoo wako pamoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *