Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Ray C amewajia juu baadhi ya mashibiki wa muziki nchini wanaomponda mwanamuziki Diamond Platnumz.

Ray C ametoa duku duku lake kupitia akaunti yake Instagram kwa kuandika maneno mazito kuhusu watu hao wanaomponda Diamond kupitia mitandao ya kijamii au vyombo vya habari hapa nchini.

Ray C ameanza kwa kuandika “Mi naumiaga sana nikiona huyu mtoto anasemwa semwa kila siku! Amefanya mapinduzi makubwa sana huyu mtoto! kama una macho unaona! Muziki wa Tanzania umefika mbali sana sababu ya watu kama hawa! Nigeria wanafika mbali sana kwa sababu wanasapotiana lakini Bongo sijui kwanini tunapenda”.

Pia akaendelea kuandika “Kuzodoana! Kushushana! Kuchukiana! Dah!! Yani huyu alieanzisha hizi social media Mungu amlaani!! #MunguakulindeDogo#DontgiveU#Mtakujakumuuamtotowawatu”

Maneno haya yanatafsiriwa kuwa yanawalenga wale wote ambao hawaoni mafanikio aliyoyaleta Diamond Platnumz katika muziki wa Bongo Fleva.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *