Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Ray C amemuomba Rais Magufuli kupitisha sheria iyakayoangalia mahusiano ya kimapenzi kati ya mwanamke na mwanaume.

Ray C alifunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram siku ya jana ambapo aliweka picha ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Mwanamuziki huyo amemuomba Rais Magufuli ahahakikishe kuwa Tanzania kuna kuwa na sheria ambayo itahahakikisha kuwa mwanaume na mwanamke wasiwe na mahusiano ya kimapenzi hadi pale watakapofunga ndoa ili wanawake wengi wapate nafasi ya kuolewa.

Ray C amefunguka hayo kwa kile alichodai kuwa wanaume wengi wana tabia ya kuchezea wasichana na wa watu na mwisho wake wanawaacha solemba bila ndoa na badala yake wanaishia kuoa wasichana wengine.

Mzee mimi nina shida moja hawa wanaume hapa nchini wanajifanya wajuaji sana! ombi langu kwako kwa mwaka huu ni hili! Naomba upitishe sheria kama ya Sultan Qaboos wa Oman! Hakuna mahusiano kati ya mwanamke na mwanaume mpaka pale watakapofunga ndoa. Na yeyote atakayekutwa na mwanamke iwe hotelini au guest house bila cheti cha ndoa wapelekwe wote segerea. Nadhani itasaidia sana kwani wanawake wengi wataolewa badala ya kuishia kuwa manungayembe! Utakuwa umewanyoosha sana hawa wanaume wetu nadhani tutaweza kuheshimiana”.

Ray C ameongea hayo kuhusu ndoa na mahusiano ingawa yeye binafsi alishaweka wazi kipindi cha nyuma kidogo kiwa kwa sasa hana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume yoyote kwani mahusiano ya kimapenzi  yamesha mpotezea sana muda wake kipindi cha nyuma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *