Kundi la mashabiki na wanachama wa Yanga wanaofahamika kama Yanga For Life leo wamewapatia zawadi wachezaji watatu wa timu hiyo ambao ni Ibrahim Ajibu, Papy Kabamba ‘Tshishimbi’ na Youthe Rostand kama motisha kutokana na mchango wao katika timu.

Kiongozi wa kundi hilo ambaye ni msanii maarufu wa filamu nchini, Vicent Kigosi maarufu kama ‘Ray’ amesema wamemzawadia Ajibu kitita cha sh milioni moja kwa kuwa mchezaji bora wa mechi mbili dhidi ya Stand United na Kagera.

kipa

Ray amesema kuwa “Sisi tunatoa zawadi kwa mchezaji bora wa kila mechi, Ajibu kachukua ya Stand na Kagera, Tshishimbi tumempa sh 500,000 pamoja na viatu na vilinda ugoko (shin guard) kwa kuibuka mchezaji bora dhidi ya Simba,”.

Mdau huyo mkubwa wa mabingwa hao mara 27 wa ligi kuu aliongeza kuwa wameamua kumpatia kipa Rostand kiasi cha sh 250,000 pamoja na viatu na shin guard kama zawadi kutokana na mchango wake kwa klabu tangu asajiliwe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *