Muigizaji wa Bongo Movie, Vicent Kigosi ‘Ray’ amemwagia sifa mzazi mwenzake Chuchu Hans kwa malezi bora ya mtoto wao Jaden.

Ray ametoa sifa hizo ikiwa ni siku ya wanawake duniani iliyoadhimishwa jana duniani kote ambapo wanawake wameungana kwa suala hilo.

Muigizaji huyo anayefahamika kwa jina la The Greatest amesema kuwa mpenzi wake huyo amekuwa msatri wa mbele katika malezi ya mtoto wao huyo Jaden aliyezaliwa mwaka jana.

Ray ameongeza kuwa kusema kuwa unajua angekuwa mwanamke mwingine angeona mtoto anamzibia vitu vingi hasa kwenye upande wa kuendelea kucheza filamu lakini aliweka pembeni lengo likawa moja tu, kumuangalia mtoto tu.

 

Pia Ray ameongeza kuwa anamuombea sana kwa Mungu mzazi mwenziye huyo aendelee kuwa na moyo huo wa malezi bora kwa mwanaye.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *