Uongozi wa klabu ya Azam FC umekubali kucheza mchezo wake wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara dhidi ya Simba kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Jumamosi hii.

 Afisa Habari wa shirikisho la soka nchini TFF, Alfred Lucas amesema TFF ilikaa na Azam na timu hiyo kuomba kuhamishia mchezo huo kutoka uwanja wa Chamazi kuja uwanja wa Uhuru.

Pia Lucas amesema kulikuwa kuna tetesi kwenye mitandao ya kijamii kuwa mchezo huo ungevurugika kutokana na kupanguliwa ratiba, kitu ambacho sio kweli.

Azam-vs-Simba-1

Hapo awali Azam FC ilitaka mchezo huo uchezwe kwenye uwanja wao wa Chamanzi uliopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam alkini TFF imeamuru mchezo huo uchezwe katika uwanja wa Uhuru.

Azam FC na Simba SC zinatarajia kukutana kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara siku ya jumamosi ambapo kila mmoja amecheza mechi nne na kushinda tatu na kutoka sare mchezo mmoja na kujikusanyia alama 10.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *