Aliyekuwa kocha msaidizi wa Hull City, Mike Phelan amechaguliwa kuwa kocha mkuu wa timu hiyo.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 53 alikuwa kocha wa muda kwenye klabu hiyo toka kuondoka kwa aliyekuwa kocha mkuu, Steve Bruce mwezi Julai mwaka huu kutokana na kutoelewana na uongozi.
Phelan ameingoza Hull City katika mechi nne za ligi kuu nchini Uingereza ambapo ameshinda mechi mbili, suluhu moja na kufungwa moja kutokana na michezo hiyo amefanikiwa kukusanya alama saba hadi sasa.
Kocha huyo toka akabidhiwe mikoba kama kocha wa muda ameonesha kuwa na kiwango kizuri mpaka uongozi umeamua kumkabidhi timu moja kwa moja kwa ajili ya kuingoza kwenye mechi za ligi kuu na mashindano mengine.
Phelan alikuwa miongoni mwa makocha waliokuwemo kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya kocha bora wa mwezi Agosti ambapo alikuwa na makocha kama Mourinho, Gurdiola na Conte huku Mourinho akiibuka na tuzo hiyo.
Hull City kesho itaikaribisha Arsenal kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uingereza itakayofanyika katika uwanja wa KCOM ukiwa ni mchezo wa tano katika ligi hiyo.