Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amewasilisha barua rasmi kwa kundi la Wasafi Classic Baby (WCB) akitaka kuvunja mkataba wake na lebo.
Kauli hiyo imesema na meneja wa kundi hilo kuwa msanii huyo ameandika barua rasmi kwa kundi hilo akisema anataka kujiondoa.
Sallam amesema kwamba kwa sasa moyo wa msanii huyo haupo tena na WCB na ameitisha mkutano na usimamizi wa WCB katika harakati yake ya kukubaliana na hatua hiyo.
Hatahivyo amesema kwamba muimbaji huyo wa wimbo ‘My Boo’ bado yupo katika mkataba wa WCB na kusisitiza kwamba ingekuwa heri iwapo Harmonise angetoka bila kuzua zahama.
Kulingana na Sallam, tangazo hilo kwamba Harmonize amejiondoa rasmi WCB litatangzwa rasmi baada ya mchakato wote huo kufuatwa na kukamilishwa.
Sallam amesema katika tamasha la wasafi lililofanyika mjini Mwanza, kwamba Harmonise alitumia usafiri wa kibinafsi kufanya baadhi ya mambo yaliotoa tafsiri kwamba amejitenga.
”Alitufanyia mambo mengi ambayo hatukutarajia ikiwemo kumsimamisha msanii ambaye hana kibali chetu. Sisi hatupendi kuleta matabaka katika kundi letu lakini kama ilivyokuwa Harmonise aliingia kivyake, sio kwamba Diamond hawezi kufanya hivyo au Rayvany ni ile heshima kwamba WCB ina umoja na kwamba tunafuata sheria zilizopo”.
Kuhusu kujitenga na wenzake Sallam amesema kwamba: Hili jambo sio sawa kulingana na maudhui ya tamasha hilo.
Maudhui ya Wasafi festival ni umoja. Msanii akiamua kuacha kuandamana na wasanii wenzake ambao wapo katika tamasha ni kwenda kinyume.
Meneja huyo amewaomba radhi wasanii wote walioshiriki tamasha la Mwanza kutokana na Harmonise kufanya jambo hilo na kwamba uongozi wa Wasafi haukuwa na taarifa.