Klabu ya Manchester United imethibitisha kumsajili mshambuliaji Romelu Lukaku kutoka Everton.
Ijumaa hii ziliibuka tetesi za Lukaku kwenda Manchester United lakini baadaye tetesi hizo zikatiliwa mashaka kwani baadhi ya vyombo vya habari vilikanusha.
Usiku wa Jumamosi taarifa mpya zikaja kwamba Chelsea wanataka kuharibu dili la United kumnunua Lukaku kwa dau sawa na ambalo United wamelipeleka Everton.
Lakini leo Mnachester United wamemaliza utata wa kuhusu Lukaku baada ya klabu hiyo kuthibitisha kwamba wametuma dau kwa Everton kumnunua Lukaku.
Katika taarifa hiyo inasema “tunafuraha kuwajulisha kwamba Everton wamekubali dau letu kwa Lukaku na sasa kilichobaki ni vipimo vya afya tu”.
Sasa kilichobaki kwa Manchestet United ni mchakato wa vipimo vya afya tu na makubaliano binafsi kuhusu mchezaji huyo ili aanze kuitumikia United.