Muigizaji kutoka nchini Nigeria, Ramsey Nouh jana amekwenda makaburi ya Kinondoni kwaajili ya kutembelea kabuli la Kunumba na kufanya ibada.
Ramsey na Mama Kanumba walitumia muda mwingi kukumbatiana na kulia kwa huzuni jambo lililoteka na kuvuta hisia za watu wengi waliofika kaburini hapo.
Pia Ramsey alizidisha machungu kwa mama huyo baada ya kuanza kutamka maneno kama anazungumza na marehemu Kanumba ambapo alimueleza mambo yenye kuumiza.
“Steven, kwa mara ya mwisho tulizungumza sote tukiwa hai lakini leo nimesimama kando yako ukiwa umelala chini ya mchanga hujitambui, kwangu ni zaidi ya msiba na kwa kweli nimeshindwa kuhimili jambo hili, najua huko uliko unaumia sana hususan ukizingatia ukweli kwamba tasnia ya filamu za Kitanzania inakufa,”.
Mazungumzo hayo ya Ramsey na Kanumba aliyoyatoa kwa hisia kali hali iliyomsababishia Mama Kanumba maumivu makali.