Muigizaji wa filamu nchini Marekani, Sylvester Stallone (Rambo) amekana ripoti kwamba yeye na mlinzi wake walimnyanyasa kingono shabiki wake wa miaka 16 mjini Las Vegas mapema miaka ya themanini.

Gazeti la mtandao la The Mail limechapisha kile linasema ni ripoti ya polisi kutoka 1986 ambayo ilielezea madai hayo.

Mwanamke huyo hakuwasilisha mashtaka dhidi ya Stallone kwa sababu alinyanyaswa na kuaibishwa mbali na kuwa na hofu.

Msemaji wa nyota huyo wa filamu ya Rocky alisema kuwa taarifa hiyo ilikuwa ya uwongo na haina ukweli wowote.

Michelle Bega aliyaelezea madai hayo kuwa ya uwongo kwa kusema kuwa hakuna mtu aliyekuwa akijua kuhusu habari hiyo hadi ilipochapishwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *