Muigizaji mkongwe wa Hollywood, Sylvester Stallone (Rambo) ameishitaki kampuni ya filamu ya Warner Bros kwa kukosa kumpa kiwango cha pesa walichokubaliana kama faida, kutokana na filamu ya mwaka 1993 ya Demolition Man.

Rambo amesema kuwa filamu hiyo ilitengeneza dola milioni 125 kwenye box office na kulingana na mkataba wake na studio hiyo, anastahili kupewa asilimia 15 ya pesa hizo.

Kampuni hiyo ya Warner Bros bado haijasema lolote kuhusu hatua hii ya kisheria iliyochukuliwa na Rambo.

Makaratasi ya kisheria ya Rambo yanaonyesha kuwa wawakilishi wake walijadili swala hilo na Warner Bros mwaka wa 2014 lakini waliarifiwa kuwa kampuni hiyo ya filamu haiwezi kumlipa chochote kwa sababu filamu ya Demolition Man ilipoteza dola milioni 66.9.

Stallone alihoji uamuzi huu na mwezi Aprili mwaka 2015 kampuni hiyo ilimtumia Stallone hundi ya dola milioni 2.8.

Kesi hii imefikishwa mbele ya mahakama ya Los Angeles na Stallone anataka ukaguzi wa pesa zote kutoka kwa filamu hiyo ufanywe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *