Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Ali Mohamed Shein amefanya mabadiliko katika Baraza la Mapinduzi huku akiongeza wizara moja zaidi.

Kwa mujibu wa taarifa Ikulu ya Zanzibar, shughuli za Vijana zimehamishiwa katika wizara mpya ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Shughli za Mazingira zimehamishiwa katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais huku shughli za Wakala wa Serikali wa Uchapaji zimehamishiwa Wizara mpya ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale.

Mabadiliko hayo yanaifanya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa na Wizara 14 zenye Mawaziri na Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:

1. OFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI

i. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi- Issa Haji Ussi Gavu

2. OFISI YA RAIS, KATIBA SHERIA, UTUMISHI WA UMMA NAUTAWALA BORA

i. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora –Haroun Ali Suleiman.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *